Omar abdalla adam tasinifu iliyowasilishwa kwa ajili ya kutimiza sharti pekee la kutunukiwa digrii ya uzamivu
Download 5.01 Kb. Pdf ko'rish
|
- Bu sahifa navigatsiya:
- 5.4.2 Mapendekezo kwa Wazazi na Wanafunzi
- 5.4.3 Mapendekezo kwa Wasomaji
- 5.4.4 Mapendekezo kwa Serikali
- VIAMBATANISHO Kiambatanisho 1: Muongozo wa Usaili kwa Wasomaji wa Riwaya Teule A: Utangulizi Mimi ninaitwa Omar Abdalla Adam
- Kuchunguza Dhamira za Kijamii na Kiutamaduni katika Riwaya ya Kiswahili: Mifano kutoka Kuli na Vuta N’kuvute
- B: Taarifa Binafsi za Msailiwa Jina……………………………… Elimu……………………………. Umri…………………………….. Kazi……………………………... C: Maswali
- Asante kwa Kunipatia Muda Wako 201 Kiambatanisho 2
- Asante kwa Kunipatia Muda Wako
5.4 Mapendekezo Mapendekezo yanayotolewa katika sehemu hii yanahusu utafiti ujao, mapendekezo kwa wazazi wa wanafunzi, wasomaji na Serikali. 5.4.1 Mapendekezo ya Utafiti Ujao Utafiti huu umefanywa kwa kutumia riwaya mbili za Kuli na Vuta N’kuvute za Shafi Adam Shafi pekee, hivyo tunapendekeza utafiti mwingine kama huu ufanywe kwa kutumia vitabu vyake vingine vya Riwaya ambavyo hatujavishughulikia. Pia, tunapendekeza utafiti wa kina ufanyike katika kutafiti matumizi ya lugha pekee katika riwaya za Shafi Adam Shafi ili kukuza zaidi yale tuliyoyatafiti sisi katika lengo mahususi la tatu la utafiti wetu. Vilevile, tunapendekeza utafiti zaidi ufanyike katika kulinganisha na kulinganua dhamira katika riwaya za Shafi Adam Shafi na zile za Mohamed Suleiman Mohamed za Nyota ya Rehema na Kiu kwa sababu zote hizi ni riwaya za Kihistoria. Pia, tunapendekeza utafiti zaidi ufanyike katika kuchunguza dhamira ya ukombozi katika riwaya za Kuli na Vuta N’kuvute. Katika utafiti huu imedokezwa tu lakini dhamira hii inaonekana kutawala katika riwaya za Shafi Adam Shafi. Hivyo, utafiti zaidi ukifanyika dhamira hii itafafanuliwa kwa kina. 5.4.2 Mapendekezo kwa Wazazi na Wanafunzi Kwa mujibu wa matokeo ya utafiti tumegundua kuwa ipo haja ya wazazi kuwapatia uhuru wa kuamua nani wa kuwa nao katika uhusiano hasa ule wa kimapenzi ili kuepusha matatizo ya kisaikolojia kama yaliyompata Yasmini. Pia, tunapendakeza kuwa ni busara kwa vijana kuwa na moyo wa uvumilivu katika ndoa zao kama ilivyokuwa kwa Amina. 189 5.4.3 Mapendekezo kwa Wasomaji Tunapendekeza kuwa, wananchi wa Tanzania kujenga utamaduni wa kujisomea kazi za fasihi hususani riwaya. Kazi za riwaya za Shafi Adam Shafi zimejaa mafunzo mazuri yenye kujenga maadili ya jamii na pia kuwapatia wasomaji uwezo mkubwa wa upeo wa kuona mbali. Ni vema kila mwanajamii anayejua kusoma akawa na nakala ya riwaya za Shafi Adam Shafi. 5.4.4 Mapendekezo kwa Serikali Tunapendekeza kuandaliwa kwa utaratibu mzuri wa uajiri katika sehemu za kazi za shurba kama bandarini ili kuepusha matatizo ya kisaikolojia kwa wafanyakazi kama makuli hasa pale wanapofikia umri mkubwa na kushindwa kufanya kazi hizo. 190 MAREJELEO Aronson, J. (1992). “A Pragmatic View of Thematic Analysis” In the Qualitative Research Methods in Nursing, Pp (37-73). Orolando FL: Grune& Stratton. Babie, E. (1999), The Basics of Social Research, Belmont: Wadsworth Publishing Company. Benner, P. (1985). “Quality of Life: A Phenomeno Logical Perspective on Explanation, Prediction and Understading in Nursing Science,” Advanees in Nursing Science, 8(1), 1-14. Beyanga, A. (2014). “Taswira ya Ng’ombe katika Nyimbo za Harusi za Jamii ya Washubi,” Tasinifu ya Uzamili, Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam. Barthes, R. (1994). The Semiotic Challenge, Berkely: University of Califonia Press. Chachage, S.C. (1991). Almasi za Bandia, Dar es Salaam University Press. Chachage, S.C. (2002). Makuadi wa Soko Huria, Dar es Salaam: E&D Company. Chandler, D. (1992). Semiotics: The Basics, London: Routledge Press. Chimerah, R.M. (1995). Nyongo Mkalia Ini, Nairobi: NUP. Chuachua, R. (2011). Itikadi katika Riwaya za Shaaban Robert, Dar es Salaam: TATAKI. Cobley, P. (2001). The Routledge Companion to Semiotics and Linguistics, London: Routledge. Cohen, L. et. al. (2000). Research Methods in Education (5 th end) London: Routledge Creswell, J.W. (2009). Research Design: Qualitative, Quantitative, and Mixed Methods Approaches, Los Angeles: SAGE Publications. 191 Diegner, L. (2011). “Mazungumzo na Adam Shafi Juu ya Uandishi wake wa Riwaya,” katika, Swahili Forum 18: 37-68. Eco, U. (1976). A Theory of Semiotics. Bloomington: Indiana University Press. Furlong, N. et.al. (2000). Research Methods and Statistics: An Intregrated Approach, New York: Hartcourt Colledge Publishers. Hawthorn, J. (1985). Studying the Novel: An Introduction, Universal Book Stall, New Delhi. Henry, G. (2011). “Uhuru wa Watumwa katika Muktadha wa Simulizi za Watumwa,” Tasinifu ya Uzamili, Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam. John, L. (2007). Critical Reading: A Guide, In http://www. Brocku. Ca/English/jlge/criticalreadig. Html. Accesssed, 30 th , October 2007. Kalegeya, T. (2013). “Utandawazi na Riwaya ya Kiswahili: Uchunguzi Kifani wa Makuadi wa Soko Huria na Almasi za Bandia,” Tasinifu ya Uzamili, Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam. Kezilahabi, E. (1971). Rosa Mistika, Dar es Salaam: DUP. Kezilahabi, E. (1976). “Shaaban Robert Mwandishi wa Riwaya,” Tasinifu ya Uzamili, Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam. Kezilahabi, E. (1983). “Utunzi wa Riwaya na Hadithi Fupi,” katika, Makala za semina ya Kimataifa ya Waandishi wa Kiswahili namba 3, Dar es Salaam: TUKI, Kur. 226-243. Kezilahabi, E. (1990). Nagona, Dar es Salaam: Dar es Salaam University Press. Kezilahabi, E. (1991). Mzingile, Dar ear es Salaam: Dar es Salaam University Press. Khamis, S.A.M. (2007). “ Utandawazi au Utandawizi?: Jinsi Lugha ya Riwaya Mpya ya Kiswahili Inavyodai,” katika Kiswahili, Juzuu namba 70, Dar es Salaam: TUKI, Kur.47-66. 192 Khatibu, M.S. (1983). “Kuli (Shafi Adam Shafi),” katika Mulika namba, 15 Dar es Salaam: TUKI, Kur. 17-24. Khatibu, M.S. (1985). “Utenzi wa Mwanakupona,” katika Mulika namba 17, Dar es Salaam: TUKI, Kur. 46-52. Khatibu, M.S. (1986). Tamathali za Semi za Kiswahili,” katika Mulika namba 18, Dar es Salaam: Tuki, Kur. 1-15. Kimbila, J. (1971). Ubeberu Utashindwa, Dar es Salaam: TUKI. King’ei, K. na Amata, J.K. (2001), Taaluma ya Ushairi, Nairobi: Acacia Stantex Publishers. Koda, B. (2000). “The Gender Dimension of Land Rights in Tanzania: Case Study of Msindo Village, Same District”, Unpublished Ph.D Thesis, UDSM. Kombo, D. K. and Tromp, D. L. A (2006). Proposal and Thesis Writing: An Introduction. Nairobi: Pauliness Publications. Kothari, C. R. (2008). Reserch Methodogy: Methods and Techiniques, New Delhi: New Age Internationl Publising Ltd. Kothari, C. R. (2004). Reserch Methodogy: Methods and Techiniques, New Delhi: New Age Internationl Publising Ltd. Kyando, L. (2013). “Majina Sadfa ya Wahusika katika Kusadikika na Kichwamaji,” katika Mulika namba, 31, TATAKI, Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, kur. 37-50. Leininger, M.M. (1985). “Ethnography and Ethnonursing: Model and Modes of Qualitative Data Analysis,” In. M.M. Leininger (Ed.). Qualitative Research Methods in Nursiny. Pp (37-73). Oro lando FL: Grune& Stratton. Lyatuu, J. (2011). “Usawiri wa Wanawake katika Fasihi ya Kiswahili: Ulinganifu wa Waandishi wa Kike na Kiume: Uchaguzi katika Riwaya Teule,” Tasnifu ya M.A. Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. 193 Madumullah, J.S. (2009). Riwaya ya Kiswahili, Historia na Misingi ya Uchambuzi, Nairobi: Sitima Printers and Stationary. Mark, G. (1995). Postmodern semiotics: Material culture and the forms of postmodern life. Oxford: Basil Blackwell. Mbatiah, M. (1998). “Mienendo Mipya katika Uandishi wa Kezilahabi: Nagona na Mzingile,” Katika Mulika namba 24, TUKI, Kur. 1-11. Mbise, I. (1996). Creative Writing. Dar es Salaam: Chuo Kikuu Huria cha Tanzania. Merrian, S. B. (1998). Qualitative Research and Case Study Applications in Education Revised and Expanded from Case Study Research in Education. San Francisco: Jossey-Bass Publishers. Mkangi, K. (1995). Walenisi, Dar es Salaam: EAEP. Mkufya, W.E. (1999). Ziraili na Zirani, Dar es Salaam: Hekima Publishers. Mjema, R. (1990). “Kusadikika,” katika Mulika namba 22, Daer es Salaam: TUKI, Kur. 26-31. Mlacha, S.A.K. (1987). “The Portrayal of Cultural Conflict in Kiswahili Prose Fiction; A Structual Study of the Novels of Euphrase Kezilahabi” Phd. Thesis, University of London. Mlacha, S.A.K. (1989). “The Use of Methaphor in Kezilahabi’s Novel: Rosa Mistika,” katika Kiswahili, Juzuu namba 56, Dar es Salaam: TUKI, Kur. 25-35. Mlacha, S.A.K. (1991). “Point of View as Stylistic Device in Kiswahili Novels,” in Kiswahili Vol. 58, Dar es Salaam: TUKI. Mlacha, S.A.K. (1996), “Utamaduni wa Mwafrika katika Riwaya ya Bwana Myombekere na Bibi Bugonoka,” katika, Mulika namba 23, Dar es Salaam: TUKI, Kur. 24-35. 194 Mlacha, S.A.K. na J.S. Madumulla, (1991). Riwaya ya Kiswahili, Dar es Salaam: Dar es Salaam University Press. Mohamed, M. (2006). Mtindo katika Riwaya ya Siku ya Watenzi Wote,” katika Kioo cha Lugha, Juzuu namba 4, Dar es Salaam: TUKI, Kur. 1-12. Mohamed, S.M. (1978). Nyota ya Rehema, Nairobi: Oxford University Press. Mohamed, S.M. (1985). Kiu, Nairobi: East African Publishing House. Mohamed, S.A. (1995). Kunga za Nathari ya Kiswahili: Riwaya, Tamthiliya na Hadithi Fupi, Nairobi: EAEP. Mohamed, S.A. (2001). Babu Alipofufuka. Nairobi: Jomo Kenyatta Foundation. Mohamed, S.A. (2006). Dunia Yao. Nairobi: Oxford University Press. Mohochi, E.S. (2000). “Usimulizi wa Riwaya ya Nyongo Mkalia Ini,” katika, Nordic Journal of African Studies, 9 (2):49-59. Momanyi, C. (2001). “Usawiri wa Wahusika wa Kike katika Fasihi ya Kiswahili baada ya mwaka 2000: Kuyumbisha Uhalisia”, katika I. S Mdee & H. J. Mwansoko: Makongamano ya Kimataifa ya Kiswahili, Dar es Salaam: TUKI. Mrikaria, S.E. (2010). “Kejeli na Fasihi ya Kiswahili Tanzania,” Katika Swahili Forum, 17: 104-125. Muhando, P. na Balisidya, N. (1976). Fasihi na Sanaa za Maonesho, Dar es Salaam: Tanzania Publishing House. Mulokozi, M.M. (1990). “Utunzi wa Riwaya ya Historia,” katika Mulika namba 22, Dar es Salaam: TUKI, Kur. 1-10. Mulokozi, M.M. (1996). Utangulizi wa Fasihi ya Kiswahili, Dar es Salaam: TUKI. 195 Mulokozi, M.M. (2013). “Makuadi wa Soko Huria (Chachage S. Chachage) katika Muktadha wa Riwaya ya Kihistoria katika Fasihi ya Kiswahili,” katika Mulika Namba, 31, TATAKI, Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, kur 51-66. Mulokozi, M.M. na Kahigi, K.K. (1979). Kunga za Ushairi na Diwani Yetu, Dar es Salaam: TPH. Msokile, M. (1992). Kunga za Fasihi na Lugha. Dar es Salaam: Education Publishers and Distributor, Ltd. Msokile, M. (1993). Miongozo ya Lugha na Fasihi: Uchambuzi na Uhakiki wa Riwaya, Dar es Salaam: DUP. Mwaifuge, E. S. (2006). “Fasihi ya Kiswahili na Rushwa Tanzania: Thomas A. R. Kamugisha na Kitu Kidogo Tu,” katika, Kioo cha Lugha, Juzuu namba, 4, Dar es Salaam: TUKI, Kur. 39-45. Mwaipopo, R. N. G. (1990). “The Impact of Commodity Relations on the Role and Status of Women in Peasant Households: A Case Study of Rungwe District”, M.A Thesis, University of Dar es Salaam. Mwangoka, N. (2011). “Motifu ya Safari na Msako katika Riwaya za Kezilahabi,” Tasinifu ya Uzamili, Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam. Nazarova, T. (1996). Linguistics and Literary Semiotics, Moscow: Moscow State University Press. Ngaiza, M.K. (2002). “Gender Dynamics in Poverty Alleviation in Tanzania: Ngara District Case Study.” Unpublished, Ph.D. Thesis, UDSM. Ngaiza, M.K. (2003). “Gender and Political Empowerment in the Third Millennium: A Conceptual Frame Work,” In Tanzania Journal of Development Studies, Vol. 4, No. 1 page 167-212. 196 Ngaiza, M.K. (2004). “Harmonization and Mainstreaming Gender in Local Government or Transforming Patriarchy: The Case of Two Wards in Bukoba District Council, Tanzania,” In Tanzania Journal of Development Studies, Vol. 5, No. 3 page 25-38. Nicholous, A. (2011). “Ubuntu katika Tamthiliya za Penina Mhando,” Tasinifu ya Uzamili, Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam. Njogu, K. na Rocha, C. (1999). Ufudishaji wa Fasihi, Nadharia na Mbinu. Nairobi: JKF. Nkwera, F.V. (1978). Sarufi na Fasihi: Sekondari na Vyuo. Dar es Salaam: Tanzania Publishing House. Nyerere, J.K. (1962). Ujamaa: The Basis of African Socialism, Dar es Salaam: Tanganyika Standard. Omary, M. (2011). “Siasa katika Ushairi wa Kezilahabi,” Tasinifu ya Uzamili, Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam. Ramadhani, S. K. (2013). “Usawiri wa Mwanamke Katika Taarab ya Mipasho: Mfano Kutoka Nyimbo za Mzee Yussuf Mzee”. Tasinifu ya M.A. Kiswahili, Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam. Robert, S. (1951). Kusadikika, London: Nelson. Robert, S. (1951). Adili na Nduguze, London: Macmillan. Robert, S. (1958). Wasifu wa Siti Binti Saad: Mwimbaji wa Unguja, London: Thomas. Robert, S. (1967). Kufikirika, Nairobi: OUP. Robert, S. (1968). Siku ya Watenzi Wote, London: Nelson. Robert, S. (1968).Utubora Mkulima, Nairobi: Nelson. 197 Robert, S. (2003). Maisha Yangu na Baada ya Miaka Hamsini, Dar es Salaam: Mkuki na Nyota Publishers. Robson, C. (2007). How to do a Reserch Project: A Guide for Undergraduate Students, Carton Victoria: Blackwell Publishing. Ruhumbika, G. (1995). Miradi Bubu ya Wazalendo, Dar es Salaam: Tanzania Publishing House. Shafi, A.S. (1978). Kasiri ya Mwinyi Fuadi, Dar es Salaam: TPH. Shafi, A.S. (1979). Kuli, Dar es Salaam: Longhorn Publishers. Shafi, A.S. (1999). Vuta N’kuvute, Dar es Salaam, Mkuki na Nyota Publishers. Shao, I.F. (2003). “Beyond Rhetoric: The Role and Experience of the University of Dar esSalaam Advancing the Involvement of Men in Gender and Development Practice,” In Tanzania Journal of Development Studies, Vol. 4 No 1. Pages 117-125. Shao, I.F. (2004). “Context for Gender Mainstreaming Internationally, Regionally and Nationally,” Paper Presented at a Gender Sensitization Workshop for UDSM Council Members, Zanzibar. Shao, I.F. (2010) .“Gender, Rural Development and Governance: An Overview”, In Tanzania Journal of Development Studies, Vol. 10 No 1 & 2 pages 78-87. Shivji, I. (2002). “Makuadi wa Soko Huria (Chachage, S. Chachage), Hotuba ya Uzinduzi wa Kitabu,” katika Mulika namba 26, 2000-2002, TUKI, Kur. 93-97, Sengo, T.S.Y.M. (1973a). “Mtu ni Utu (G. Mhina),” katika Hisi Zetu, Dar es Salaam: TUKI. Sengo, T.S.Y.M. (1973b), “Dhima ya Fasihi kwa Maendeleo ya Jamii,” katika Jarida la Kiswahili, Dar es Salaam: TUKI. 198 Sengo, T.S.Y.M. (1987). Fasihi Simulizi, Sekondari na Vyuo: Dar es Salaam: Nyanza Publications Agency. Sengo, T.S.Y.M. (2009). Sengo na Fasihi za Kinchi. Dar es Salaam: AKADEMIYA Sengo, T.S.Y.M. (2014). Falsafa ya Maisha, Dar es Salaam: Hakijachapishwa. Sengo, T.S.Y.M. na Kiango, S.D. (2012). Hisiya Zetu, Dar es Salaam: TUKI. Senkoro, F.E.M.K. (1977). “Riwaya ya Kiswahili na Maendeleo ya Umma,” Tasinifu ya Uzamili, Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam. Senkoro, F.E.M.K. (1976). “Utamaduni katika Riwaya za Kiswahili,” katika Kiswahili, Juzuu namba 46/2, Dar es Salaam: TUKI, Kur. 74-82. Senkoro, F.M.E.K., (1982). Fasihi. Dar es Salaam: DUP. Senkoro, F.E.M.K. (1997). “The Significance of Journey in Zanzibar Forktales,” Unpublished Ph.D Thesis, University of Dar es Salaam. Senkoro, F.E.M.K., (2006). “Fasihiya Kiswahili ya Majaribio: Makutano baina ya Fasihi Simulizi na Fasihi Andishi”, katika, Kioo cha Lugha, Juzuu, 1. Idara ya Kiswahili Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam uk. 61-68. Senkoro, F.E.M.K. (2011). Fasihi Andishi. Dar es Salaam: KAUTTU. Swahili Tittles, (2011). “Book Collective,” Searched on www.africanbooks collective.com. On Monday 26/01/2012, at 12:23 Hours. Taib, A.H., (2008). “Mkabala wa Kiislamu katika Uchanganuzi na uhakiki wa Fasihi ya Kiswahili,” CHAKAMA, kur. 133-141. Taylor, S.J. & Bogdan. R., (1984). Introduction to Qualitative Research Methods: The Search for Meanings. New York: John Wiley& Sons. Walibora, K.W. (2010). “Uhalisia na Uhalisiamazingaombwe: Mshabaha kati ya Duniya Yao na The Tin Drum,” katika, Swahili Forum 17:143-157. 199 Walibora, K.W. (2013). “Ujasiri wa Kujimulika katika Uandishi wa Kiswahili: Uhakiki wa Mbali na Nyumbani,” Tawasifu ya Shafi Adam Shafi. Wamitila, K.W. (2002). Uhakiki wa Fasihi: Misingi na Vipengele Vyake, Nairobi: Phoenix Publishers Ltd. Wamitila, (2002). Bina-Adamu, Nairobi: Phoenix Publishers. Wamitila, K.W. (2003). “Influence or Intertextuality? A Comparative Study of Kezilahabi’s Nagona and Mzingile and Juan Rulfo’s Pedro Paramo,” in Kiswahili Vol. 66, pp. 49-58. Wamitila, K.W. (2007). “Narative Structure and Metaphor: Towards a new Aesthetics of the Kiswahili Novel,” in Kiswahili Vol. 70, Dar es Salaam: IKS, Pp. 67-75. Wamitila, K.W., (2008). Kanzi ya Fasihi: Misingi ya Uchanganuzi wa Fasihi, Nairobi: Vide-Muwa. Wamitila, K.W. (2013). “Mikakati ya Uhalisiajabu katika Riwaya ya Kiswahili,” katika Mulika namba, 32, TATAKI: Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam. Wanyonyi, M.C. (2011). “Uhakiki wa Riwaya ya Nyunso za Mwanamke na Said Ahmed Mohamed: Mtazamo wa Saikolojia Changanuzi,” Tasinifu ya Uzamivu, Chuo Kikuu Cha Nairobi. Yin, R. K., (1994). Case Study Research: Design and Methods, (2 nd eds.) Thousand Oaks Calif: SAGE Publishers. Young, P.V. (1984). Scientific Social Surves and Research, Englewood Chiffs: Prentice Hall. Inc. 200 VIAMBATANISHO Kiambatanisho 1: Muongozo wa Usaili kwa Wasomaji wa Riwaya Teule A: Utangulizi Mimi ninaitwa Omar Abdalla Adam mwanafunzi wa Shahada ya Uzamivu (Ph.D) katika Kiswahili katika Chuo Kikuu Huria Cha Tanzania. Ninafanya Utafiti wenye anuani isemayo Kuchunguza Dhamira za Kijamii na Kiutamaduni katika Riwaya ya Kiswahili: Mifano kutoka Kuli na Vuta N’kuvute. Ili niweze kupata data za kuweza kukamilisha utafiti huu nimeandaa muongozo huu ambao ndani yake kuna maswali yaliyolengwa kwako na ninaomba nikufanyie usaili. B: Taarifa Binafsi za Msailiwa Jina……………………………… Elimu……………………………. Umri…………………………….. Kazi……………………………... C: Maswali 1. Naomba unieleze vile ulivyopata kumfahamu Shafi Adam Shafi. 2. Taja riwaya za Shafi Adam Shafi unazozifahamu? 3. Ni zipi kati ya Riwaya hizo umeshazisoma? 4. Ni riwaya ipi iliyokuvutia zaidi? Toa sababu kwa jibu lako. 5. Orodhesha dhamira ulizozipata katika usomaji wako wa kazi za Shafi Adam Shafi. 6. Suala la ndoa za Kulazimishwa likoje katika jamii ya sasa ukilinganisha na ilivyo katika Vuta N’kuvute? 7. Suala la kupata na kutopata mtoto baada ya ndoa linatazamwaje katika jamii ya sasa? 8. Ni upi mtazamo wa jamii ya leo kuhusiana na umuhimu wa elimu ikilinganishwa na inavyoelezwa katika Kuli? 9. Mabadiliko ya utamaduni wa jamii ya Unguja kuhusu mke na mume yanasabaibishwa na nini? 10. Naomba unieleze jambo lolote ambalo ni muhimu kuhusu riwaya za Shafi Adam Shafi ambalo nimesahau kukuuliza. Asante kwa Kunipatia Muda Wako 201 Kiambatanisho 2: Muongozo wa Usaili kwa Wataalamu wa Fasihi A: Utangulizi Mimi ninaitwa Omar Abdalla Adam mwanafunzi wa Shahada ya Uzamivu (Ph.D) katika Kiswahili katika Chuo Kikuu Huria Cha Tanzania. Ninafanya Utafiti wenye anuani isemayo Kuchunguza Dhamira za Kijamii na Kiutamaduni katika Riwaya ya Kiswahili: Mifano kutoka Kuli na Vuta N’kuvute. Ili niweze kupata data za kuweza kukamilisha utafiti huu nimeandaa muongozo huu ambao ndani yake kuna maswali yaliyolengwa kwako na ninaomba nikufanyie usaili. B: Taarifa Binafsi za Msailiwa Jina……………………………… Elimu……………………………. Umri…………………………….. Kazi……………………………... C: Maswali 1. Naomba unieleze vile ulivyopata kumfahamu Shafi Adam Shafi. 2. Taja riwaya za Shafi Adam Shafi unazozifahamu? 3. Ni zipi kati ya Riwaya hizo umeshazisoma? 4. Ni riwaya ipi iliyokuvutia zaidi? Toa sababu kwa jibu lako. 5. Orodhesha dhamira ulizozipata katika usomaji wako wa kazi za Shafi Adam Shafi. 6. Taja mbinu za kisanaa zinazotumiwa na Shafi Adam Shafi katika kujenga dhamira za riwaya zake? 7. Kati ya Kuli na Vuta N’kuvute ni ipi inayokuvutia zaidi? 8. Kwa nini Shafi Adam Shafi anapenda mno kutumia barua katika riwaya zake? 9. Shafi Adam Shafi anatumia motifu za aina gani katika Kuli na Vuta N,kuvute? Motifu hizo zina dhima gani? 10. Naomba unieleze jambo lolote ambalo ni muhimu kuhusu riwaya za Shafi Adam Shafi ambalo nimesahau kukuuliza. Asante kwa Kunipatia Muda Wako Download 5.01 Kb. Do'stlaringiz bilan baham: |
Ma'lumotlar bazasi mualliflik huquqi bilan himoyalangan ©fayllar.org 2024
ma'muriyatiga murojaat qiling
ma'muriyatiga murojaat qiling